Mwanafunzi
wa Mwaka wa Kwanza Uhandisi wa Kompyuta wa chuo cha Usimamizi wa Fedha
(IFM) Wendy Habakuki Lwendo amefariki dunia katika ufukwe wa bahari ya
Hindi eneo la Kipepeo Kigamboni akiogelea na wenzake watatu jana jioni.Akizungumza
na Father Kidevu Blog, kaka wa Marehemu, Sammy Lwendo amesema mdogo wao
alipatwa na maswahibu hayo akiwa na rafiki zake hao watatu wakiogelea
baharini na wakati wanaogelea walikuwa katika eneo la kina kifupi cha
maji yaliyokupwa na mara maji hayo yaka jaa na walipokuwa wakijaribu
kutoka ndipo Wendy akazidiwa na maji.
Lwendo amesema kuwa wenzake walifanikiwa kumtoa majini lakini hali yake
tayari ilikuwa mbaya na kwakuwa hawakuwa na ujuzi wa kutosha wa kutoa
huduma ya kwanza kwa mtu aliyezama majini walihangaika kwa zaidi ya
dakika 40 kumsaidia ndipo wakapata msaada wa Polisi kumkimbiza kituo cha
afya Kibaoni huko Kigamboni lakini jitihada za kuokoa maisha yake
ziligonga mwamba.Aidha alisema kuwa mwili wa Marehemu ulihamishiwa
katika Hospitali ya Wilaya Vijibweni na sasa ndugu wamefika na
kuhamishia mwili huo Hospitali ya jeshi Lugalo.Msiba kwa sasa upo
Kinondoni nyuma ya Vijana, huku wakisubiriwa wazazi wa marehemu pamoja
na ndugu wengine ili kujua taratibu kamili za maziko.
Wazazi wa Wendy, Mchungaji Habakuki Lwendo ni mwalimu wa Chuo cha Uchungaji Makumira mkoani Arusha.

No comments:
Post a Comment