Friday, 21 June 2013

           NAHODHA AWATAKA WAUMINI WA DINI YA KISLAMU KUBADILIKA
                     WATUMIE MIKUSANYIKO YAO KUELEKEZA NJIA ZA UCHUMI.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha amewataka waumini wa Dini ya Kislamu kuitumia mikusanyiko yao katika kuelekezana njia bora za kupambana na umasikini miongoni mwa jamii ilikujiondoa na dhana kuwa wao ni watu wanyonge.

Amesema umoja na mshikamano miongoni mwao ninjia maridhawa ya kuwapatia maendeleo endapo mikusanyiko yao kama ya ijitimai wataitumia vyema badala ya kuhofishana kutotenda mbaya ilikupta Pepo basi pia waelekezane kufanya vizuri ilikuondokana na umasikini.

Amesema iletabia ilio jengeka ya kumtambua muislamu kwa kuvaa kanzu mbovu na kofia ilio choka imepitwa na wakati bali waislamu wazitumie fursa na vipao mbele vya nchi ilikujipatia maendeleo sawa na wengine katika taifa lao


"Haya ya maendeleo jamani yatakuja kama sote tukikubali kuwa nakiongozi mwenye sauti moja na kuwa na umoja na kutumia umoja wetu katika kutafuta maendeleo "alisema nahodha.

Aidha muhismiwa Nahodha aliwataka waumini wa dini ya kislamu kujikita katika kutafuta elimu kwani alisema inasikitisha kuona hadi asasa ndani ya Tanzania hadi asasa kuna chuo kimoja tu cha waislamu wakati watu wa dini nyengine wana vyuo vikuu zaidi ya sita .

No comments:

Post a Comment