Aidha kufuatia ajali hiyo, watu kumi wamejeruhiwa na kupelekwa hospitali
kwa ajili ya matibabu, watatu kati yao wamepelekwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Kongwa. Majeruhi hao wote watatu ni wa kiume wametajwa kuwa ni
Rabiel Masue (27), Mkazi wa Mwenge Dar es Salaam, Charles Joseph (28)
Mkazi Kapri Point, Mwanza na Burton Kimaro (27) Mkazi wa Mwanza.Alisema
majeruhi wengine saba ambapo watatu kati yao wakiwa ni wanawake
wanatibiwa katika Hospitali ya Rufaa Dodoma.Kufuatia tukio hili la
ajali, Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo na
wote watakapopatikana na makosa watafikishwa mbele ya sheria.Kaimu
Kamanda alisema Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa rai kwa madereva
hususan wa magari ya abiria kuzingatia miiko na maadili ya udereva na
kutoenda mwendokasi. Aidha linawataka abiria, iwapo dereva atakuwa
anakwenda mwendokasi, watoe taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi ili
hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma
linawaomba wamiliki wa vyombo vya usafiri wanapowaajiri madereva,
wahakikishe kuwa wamewasaili kikamilifu na wanakidhi vigezo
vinavyohitajika kisheria.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Dodoma
Dk,Nassoro Mzee alisema majeruhi walianz kupokelewa kuanzia saa nane
mchana jana.Kwa upande wao majeruhi waliyolazwa kwenye hospital hiyo
walisema kuwa chanzo cha ajali ni kupasukaa kwa tairi la mbele na wakati
huo dereva alikuwa mwendokasi.Mmoja wa majeruhi John Kazungu (25)
alisema kuwa licha ya pancha lakini pia dereva alikuwa katika mwendo wa
kasi hali iliyosababisha ajali hiyo.
“ Mimi Nilikuwa upande wa Kondakta mara nikasiki kishindo kikubwa na
kuanza kuona gari yetu ikaacha kwa kupoteza muelekeo wa njia na
kupinduka toka hapa sikujua kinacho endelea ndio nimejikuta hapa, ”
alisema Kazungu
No comments:
Post a Comment